17. Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu,Na wale walionichukia,Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.
18. Walinikabili siku ya msiba wangu,Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu.
19. Akanitoa akanipeleka panapo nafasi,Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
20. BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu,Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.
21. Maana nimezishika njia za BWANA,Wala sikumwasi Mungu wangu.
22. Hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu,Wala amri zake sikujiepusha nazo.
23. Nami nalikuwa mkamilifu mbele zake,Nikajilinda na uovu wangu.
24. Mradi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu,Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.
25. Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili;Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;
26. Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu;Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi.
27. Maana Wewe utawaokoa watu wanaoonewa,Na macho ya kiburi utayadhili.
28. Kwa kuwa Wewe unaiwasha taa yangu;BWANA Mungu wangu aniangazia giza langu.
29. Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi,Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta.
30. Mungu, njia yake ni kamilifu,Ahadi ya BWANA imehakikishwa,Yeye ndiye ngao yao.Wote wanaomkimbilia.
31. Maana ni nani aliye Mungu ila BWANA?Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu?
32. Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu,Naye anaifanya kamilifu njia yangu.
33. Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu,Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.
34. Ananifundisha mikono yangu vita,Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba.
35. Nawe umenipa ngao ya wokovu wako,Mkono wako wa kuume umenitegemeza,Na unyenyekevu wako umenikuza.