Zab. 18:17-24 Swahili Union Version (SUV)

17. Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu,Na wale walionichukia,Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.

18. Walinikabili siku ya msiba wangu,Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu.

19. Akanitoa akanipeleka panapo nafasi,Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.

20. BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu,Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.

21. Maana nimezishika njia za BWANA,Wala sikumwasi Mungu wangu.

22. Hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu,Wala amri zake sikujiepusha nazo.

23. Nami nalikuwa mkamilifu mbele zake,Nikajilinda na uovu wangu.

24. Mradi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu,Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.

Zab. 18