16. Alipeleka kutoka juu akanishika,Na kunitoa katika maji mengi.
17. Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu,Na wale walionichukia,Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.
18. Walinikabili siku ya msiba wangu,Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu.
19. Akanitoa akanipeleka panapo nafasi,Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
20. BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu,Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.