8. Unilinde kama mboni ya jicho,Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
9. Wasinione wasio haki wanaonionea,Adui za roho yangu wanaonizunguka.
10. Wameukaza moyo wako,Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.
11. Sasa wametuzunguka hatua zetu,Na kuyakaza macho yao watuangushe chini.
12. Kama mfano wa simba atakaye kurarua,Kama mwana-simba aoteaye katika maoteo yake.
13. Ee BWANA, usimame, umkabili, umwinamishe,Kwa upanga wako uniokoe nafsi na mtu mbaya.
14. Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu,Watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya.Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako,Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,