Zab. 145:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza,Nitalihimidi jina lako milele na milele.

2. Kila siku nitakuhimidi,Nitalisifu jina lako milele na milele.

3. BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,Wala ukuu wake hautambulikani.

4. Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako,Kitayatangaza matendo yako makuu.

5. Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako,Na matendo yako yote ya ajabu.

6. Watu watayataja matendo yako ya kutisha,Nami nitausimulia ukuu wako.

Zab. 145