1. Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA,Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.
2. Nitafunua mbele zake malalamiko yangu,Shida yangu nitaitangaza mbele zake.
3. Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu;Katika njia niendayo wamenifichia mtego.
4. Utazame mkono wa kuume ukaone,Kwa maana sina mtu anijuaye.Makimbilio yamenipotea,Hakuna wa kunitunza roho.