1. Ee BWANA, nimekuita, unijie hima,Uisikie sauti yangu nikuitapo.
2. Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba,Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
3. Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu,Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.
4. Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya,Nisiyazoelee matendo yasiyofaa,Pamoja na watu watendao maovu;Wala nisile vyakula vyao vya anasa.
5. Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili;Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani;Kichwa changu kisikatae,Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.
6. Makadhi wao wakiangushwa kando ya genge,Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu.