3. Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja,Hakuna atendaye mema,La! Hata mmoja.
4. Je! Wote wafanyao maovu hawajui?Walao watu wangu kama walavyo mkate,Hawamwiti BWANA.
5. Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi,Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.
6. Mnalitia aibu shauri la mtu mnyonge,Bali BWANA ndiye aliye kimbilio lake.