Zab. 139:5-11 Swahili Union Version (SUV)

5. Umenizingira nyuma na mbele,Ukaniwekea mkono wako.

6. Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi,Hayadirikiki, siwezi kuyafikia.

7. Niende wapi nijiepushe na roho yako?Niende wapi niukimbie uso wako?

8. Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko;Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.

9. Ningezitwaa mbawa za asubuhi,Na kukaa pande za mwisho za bahari;

10. Huko nako mkono wako utaniongoza,Na mkono wako wa kuume utanishika.

11. Kama nikisema, Hakika giza litanifunika,Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;

Zab. 139