Zab. 139:2-5 Swahili Union Version (SUV)

2. Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;Umelifahamu wazo langu tokea mbali.

3. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,Umeelewa na njia zangu zote.

4. Maana hamna neno ulimini mwanguUsilolijua kabisa, BWANA.

5. Umenizingira nyuma na mbele,Ukaniwekea mkono wako.

Zab. 139