Zab. 132:2-10 Swahili Union Version (SUV)

2. Ndiye aliyemwapia BWANA,Akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo.

3. Sitaingia hemani mwa nyumba yangu,Wala sitapanda matandiko ya kitanda changu;

4. Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi,Wala kope zangu kusinzia;

5. Hata nitakapompatia BWANA mahali,Na Shujaa wa Yakobo maskani.

6. Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata,Katika konde la Yearimu tuliiona.

7. Na tuingie katika maskani yake,Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake.

8. Ee BWANA, uinuke, uende kwenye raha yako,Wewe na sanduku la nguvu zako.

9. Makuhani wako na wavikwe haki,Watauwa wako na washangilie.

10. Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako,Usiurudishe nyuma uso wa masihi wako.

Zab. 132