1. BWANA, umkumbukie DaudiTaabu zake zote alizotaabika.
2. Ndiye aliyemwapia BWANA,Akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo.
3. Sitaingia hemani mwa nyumba yangu,Wala sitapanda matandiko ya kitanda changu;
4. Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi,Wala kope zangu kusinzia;
5. Hata nitakapompatia BWANA mahali,Na Shujaa wa Yakobo maskani.