4. Lakini kwako kuna msamaha,Ili Wewe uogopwe.
5. Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja,Na neno lake nimelitumainia.
6. Nafsi yangu inamngoja Bwana,Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,Naam, walinzi waingojao asubuhi.
7. Ee Israeli, umtarajie BWANA;Maana kwa BWANA kuna fadhili,Na kwake kuna ukombozi mwingi.