Zab. 130:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia.

2. Bwana, uisikie sauti yangu.Masikio yako na yaisikilizeSauti ya dua zangu.

3. BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu,Ee Bwana, nani angesimama?

4. Lakini kwako kuna msamaha,Ili Wewe uogopwe.

5. Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja,Na neno lake nimelitumainia.

Zab. 130