2. Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,Wanadamu walipotushambulia.
3. Papo hapo wangalitumeza hai,Hasira yao ilipowaka juu yetu
4. Papo hapo maji yangalitugharikisha,Mto ungalipita juu ya roho zetu;
5. Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetuMaji yafurikayo.
6. Na ahimidiwe BWANA;Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.