1. Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,Israeli na aseme sasa,
2. Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,Wanadamu walipotushambulia.
3. Papo hapo wangalitumeza hai,Hasira yao ilipowaka juu yetu
4. Papo hapo maji yangalitugharikisha,Mto ungalipita juu ya roho zetu;