Zab. 12:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. BWANA, uokoe, maana mcha Mungu amekoma,Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.

2. Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe,Wenye midomo ya kujipendekeza;Husemezana kwa mioyo ya unafiki;

3. BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza,Nao ulimi unenao maneno ya kiburi;

4. Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda;Midomo yetu ni yetu wenyewe,Ni nani aliye bwana juu yetu?

5. Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge,Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji,Sasa nitasimama, asema BWANA,Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.

Zab. 12