4. BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5. Ni nani aliye mfano wa BWANA,Mungu wetu aketiye juu;
6. Anyenyekeaye kutazama,Mbinguni na duniani?
7. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8. Amketishe pamoja na wakuu,Pamoja na wakuu wa watu wake.