5. Amewapa wamchao chakula;Atalikumbuka agano lake milele.
6. Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake,Kwa kuwapa urithi wa mataifa.
7. Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu,Maagizo yake yote ni amini,
8. Yamethibitika milele na milele,Yamefanywa katika kweli na adili.
9. Amewapelekea watu wake ukombozi,Ameamuru agano lake liwe la milele,Jina lake ni takatifu la kuogopwa.