7. Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki,Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.
8. Siku zake na ziwe chache,Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.
9. Wanawe na wawe yatima,Na mkewe na awe mjane.
10. Kutanga na watange wanawe na kuomba,Watafute chakula mbali na mahame yao.
11. Mdai na anase vitu vyote alivyo navyo,Wageni na wateke mapato ya kazi yake.
12. Asiwe na mtu wa kumfanyia fadhili,Wala mtu wa kuwahurumia yatima wake.
13. Wazao wake waangamizwe,Jina lao likafutwe katika kizazi cha pili.
14. Uovu wa baba zake ukumbukwe mbele za BWANA,Na dhambi ya mamaye isifutwe.
15. Ziwe mbele za BWANA daima,Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
16. Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili,Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji,Hata akamfisha mtu aliyevunjika moyo,
17. Naye alipenda kulaani, nako kukampata.Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye,
18. Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake.Ikamwingilia moyoni kama maji,Na kama mafuta mifupani mwake.