Zab. 109:16-27 Swahili Union Version (SUV)

16. Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili,Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji,Hata akamfisha mtu aliyevunjika moyo,

17. Naye alipenda kulaani, nako kukampata.Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye,

18. Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake.Ikamwingilia moyoni kama maji,Na kama mafuta mifupani mwake.

19. Na iwe kwake kama vazi ajivikalo,Na kama mshipi ajifungao daima.

20. Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa BWANA,Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.

21. Na Wewe, MUNGU, Bwana, unitendee kwa ajili ya jina lako,Kwa kuwa fadhili zako ni njema uniokoe.

22. Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji,Na moyo wangu umejeruhi ndani yangu.

23. Ninapita kama kivuli kianzacho kutoweka,Ninapeperushwa kama nzige.

24. Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga,Na mwili wangu umekonda kwa kukosa mafuta.

25. Nami nalikuwa laumu kwao,Wanionapo hutikisa vichwa vyao.

26. Ee BWANA, Mungu wangu, unisaidie,Uniokoe sawasawa na fadhili zako.

27. Nao wakajue ya kuwa ndio mkono wako;Wewe, BWANA, umeyafanya hayo.

Zab. 109