Zab. 106:2-13 Swahili Union Version (SUV)

2. Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA,Kuzihubiri sifa zake zote?

3. Heri washikao hukumu,Na kutenda haki sikuzote.

4. Ee BWANA, unikumbuke mimi,Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.Unijilie kwa wokovu wako,

5. Ili niuone wema wa wateule wako.Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako,Na kujisifu pamoja na watu wako.

6. Tumetenda dhambi pamoja na baba zetu,Tumetenda maovu, tumefanya ubaya.

7. Baba zetu katika MisriHawakufikiri matendo yako ya ajabu;Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako;Wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu.

8. Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake,Ayadhihirishe matendo yake makuu.

9. Akaikemea bahari ya Shamu ikakauka,Akawaongoza vilindini kana kwamba ni uwanda.

10. Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia,Na kuwakomboa na mkono wa adui zao.

11. Maji yakawafunika watesi wao,Hakusalia hata mmoja wao.

12. Ndipo walipoyaamini maneno yake,Waliziimba sifa zake.

13. Wakayasahau matendo yake kwa haraka,Hawakulingojea shauri lake.

Zab. 106