Zab. 104:19-32 Swahili Union Version (SUV)

19. Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati,Jua latambua kuchwa kwake.

20. Wewe hufanya giza, kukawa usiku,Ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu.

21. Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo,Ili kutafuta chakula chao kwa Mungu.

22. Jua lachomoza, wanakwenda zao,Na kujilaza mapangoni mwao.

23. Mwanadamu atoka kwenda zake kazini,Na kwenye utumishi wake mpaka jioni.

24. Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako!Kwa hekima umevifanya vyote pia.Dunia imejaa mali zako.

25. Bahari iko kule, kubwa na upana,Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika,Viumbe hai vidogo kwa vikubwa.

26. Ndimo zipitamo merikebu,Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo.

27. Hao wote wanakungoja Wewe,Uwape chakula chao kwa wakati wake.

28. Wewe huwapa,Wao wanakiokota;Wewe waukunjua mkono wako,Wao wanashiba mema;

29. Wewe wauficha uso wako,Wao wanafadhaika;Waiondoa pumzi yao, wanakufa,Na kuyarudia mavumbi yao,

30. Waipeleka roho yako, wanaumbwa,Nawe waufanya upya uso wa nchi.

31. Utukufu wa BWANA na udumu milele;BWANA na ayafurahie matendo yake.

32. Aitazama nchi, inatetemeka;Aigusa milima, inatoka moshi.

Zab. 104