Zab. 104:1-16 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.Wewe, BWANA, Mungu wangu,Umejifanya mkuu sana;Umejivika heshima na adhama.

2. Umejivika nuru kama vazi;Umezitandika mbingu kama pazia;

3. Na kuziweka nguzo za orofa zake majini.Huyafanya mawingu kuwa gari lake,Na kwenda juu ya mabawa ya upepo,

4. Huwafanya malaika zake kuwa pepo,Na watumishi wake kuwa moto wa miali.

5. Uliiweka nchi juu ya misingi yake,Isitikisike milele.

6. Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi,Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima.

7. Kwa kukemea kwako yakakimbia,Kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi,

8. Yakapanda milima, yakatelemka mabondeni,Mpaka mahali ulipoyatengenezea.

9. Umeweka mpaka yasiupite,Wala yasirudi kuifunikiza nchi.

10. Hupeleka chemchemi katika mabonde;Zapita kati ya milima;

11. Zamnywesha kila mnyama wa kondeni;Punda mwitu huzima kiu yao.

12. Kandokando hukaa ndege wa angani;Kati ya matawi hutoa sauti zao.

13. Huinywesha milima toka orofa zake;Nchi imeshiba mazao ya kazi zako.

14. Huyameesha majani kwa makundi,Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu;Ili atoe chakula katika nchi,

15. Na divai imfurahishe mtu moyo wake.Aung’aze uso wake kwa mafuta,Na mkate umburudishe mtu moyo wake.

16. Miti ya BWANA nayo imeshiba,Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.

Zab. 104