Zab. 103:6-12 Swahili Union Version (SUV)

6. BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki,Na hukumu kwa wote wanaoonewa.

7. Alimjulisha Musa njia zake,Wana wa Israeli matendo yake.

8. BWANA amejaa huruma na neema,Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.

9. Yeye hatateta sikuzote,Wala hatashika hasira yake milele.

10. Hakututenda sawasawa na hatia zetu,Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.

11. Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.

12. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

Zab. 103