Zab. 103:11-16 Swahili Union Version (SUV)

11. Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.

12. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

13. Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao.

14. Kwa maana Yeye anatujua umbo letu,Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.

15. Mwanadamu siku zake zi kama majani;Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo.

16. Maana upepo hupita juu yake, kumbe haliko!Na mahali pake hapatalijua tena.

Zab. 103