1. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.Naam, vyote vilivyo ndani yanguVilihimidi jina lake takatifu.
2. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA,Wala usizisahau fadhili zake zote.
3. Akusamehe maovu yako yote,Akuponya magonjwa yako yote,
4. Aukomboa uhai wako na kaburi,Akutia taji ya fadhili na rehema,
5. Aushibisha mema uzee wako,Ujana wako ukarejezwa kama tai;
6. BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki,Na hukumu kwa wote wanaoonewa.
7. Alimjulisha Musa njia zake,Wana wa Israeli matendo yake.