Zab. 102:5-13 Swahili Union Version (SUV)

5. Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwanguMifupa yangu imegandamana na nyama yangu.

6. Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,Na kufanana na bundi wa mahameni.

7. Nakesha, tena nimekuwa kama shomoroAliye peke yake juu ya nyumba.

8. Adui zangu wananilaumu mchana kutwa;Wanaonichukia kana kwamba wana wazimuHuapa kwa kunitaja mimi.

9. Maana nimekula majivu kama chakula,Na kukichanganya kinywaji changu na machozi.

10. Kwa sababu ya ghadhabu yako na hasira yako;Maana umeniinua na kunitupilia mbali.

11. Siku zangu zi kama kivuli kilichotandaa,Nami ninanyauka kama majani.

12. Bali Wewe, BWANA utaketi ukimiliki milele,Na kumbukumbu lako kizazi hata kizazi.

13. Wewe mwenyewe utasimama,Na kuirehemu Sayuni,Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia,Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.

Zab. 102