11. Siku zangu zi kama kivuli kilichotandaa,Nami ninanyauka kama majani.
12. Bali Wewe, BWANA utaketi ukimiliki milele,Na kumbukumbu lako kizazi hata kizazi.
13. Wewe mwenyewe utasimama,Na kuirehemu Sayuni,Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia,Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.
14. Maana watumishi wako wameyaridhia mawe yake,Na kuyaonea huruma mavumbi yake.
15. Kisha mataifa wataliogopa jina la BWANA,Na wafalme wote wa dunia utukufu wako;
16. BWANA atakapokuwa ameijenga Sayuni,Atakapoonekana katika utukufu wake,
17. Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,Asiyadharau maombi yao.
18. Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo,Na watu watakaoumbwa watamsifu BWANA.
19. Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu,Toka mbinguni BWANA ameiangalia nchi,
20. Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa,Na kuwafungua walioandikiwa kufa.
21. Watu walitangaze jina la BWANA katika Sayuni,Na sifa zake katika Yerusalemu,
22. Pindi mataifa watapokusanyika pamoja,Falme nazo ili kumtumikia BWANA.