6. Asema moyoni mwake, Sitaondoshwa,Kizazi baada ya kizazi sitakuwamo taabuni.
7. Kinywa chake kimejaa laana,Na hila na dhuluma.Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu,
8. Hukaa katika maoteo ya vijiji.Mahali pa siri humwua asiye na hatia,Macho yake humvizia mtu duni.
9. Huotea faraghani kama simba pangoni,Huotea amkamate mtu mnyonge.Naam, humkamata mtu mnyonge,Akimkokota wavuni mwake.
10. Hujikunyata na kuinama;Watu duni huanguka kwa nguvu zake.
11. Asema moyoni mwake, Mungu amesahau,Auficha uso wake, haoni kamwe.
12. BWANA, uondoke, Ee Mungu, uuinue mkono wako,Usiwasahau wanyonge.
13. Kwani mdhalimu kumdharau Mungu.Akisema moyoni mwake, Hutapatiliza?