Zab. 10:11-17 Swahili Union Version (SUV)

11. Asema moyoni mwake, Mungu amesahau,Auficha uso wake, haoni kamwe.

12. BWANA, uondoke, Ee Mungu, uuinue mkono wako,Usiwasahau wanyonge.

13. Kwani mdhalimu kumdharau Mungu.Akisema moyoni mwake, Hutapatiliza?

14. Umeona, maana unaangalia madhara na jeuri,Uyatwae mkononi mwako.Mtu duni hukuachia nafsi yake,Maana umekuwa msaidizi wa yatima.

15. Uuvunje mkono wake mdhalimu,Na mbaya, uipatilize dhuluma yake, hata usiione.

16. BWANA ndiye Mfalme milele na milele;Mataifa wamepotea kutoka nchi yake.

17. BWANA, umeisikia tamaa ya wanyonge,Utaitengeneza mioyo yao, utalitega sikio lako.

Zab. 10