7. Basi, kwa hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu; maana nisipotenda hivi, nitende nini kwa ajili ya binti ya watu wangu?
8. Ulimi wao ni mshale ufishao; husema maneno ya hadaa; mtu mmoja husema maneno ya amani na mwenzake kwa kinywa chake, lakini moyoni mwake humwotea.
9. Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?
10. Kwa milima nitalia na kulalama,Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo;Kwa sababu yameteketea, hata hapana apitaye,Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng’ombe;Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni,Wamekimbia, wamekwenda zao.
11. Nami nitafanya Yerusalemu kuwa magofu,Makao ya mbweha;Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa,Isikaliwe na mtu awaye yote.