Yer. 50:36-43 Swahili Union Version (SUV)

36. Upanga u juu ya hao wajisifuo, nao watapumbazika; upanga u juu ya mashujaa wake, nao watafadhaika.

37. Upanga u juu ya farasi zao, na juu ya magari yao ya vita; na juu ya watu wote waliochanganyika ndani yake, nao watakuwa kama wanawake; upanga u juu ya hazina zake, nazo zitaibwa.

38. Ukosefu wa mvua u juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu.

39. Basi, wanyama wakali wa jangwani, pamoja na mbwa-mwitu, watakaa huko, na mbuni watakaa ndani yake; wala haitakaliwa na watu milele; wala hapana mtu atakayekaa huko tangu kizazi hata kizazi.

40. Kama vile vilivyotokea Mungu alipoangusha Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema BWANA; kadhalika hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama wageni wakaavyo.

41. Angalia, watu wanakuja watokao kaskazini; na taifa kubwa, na wafalme wengi wataamshwa toka pande za mwisho za dunia.

42. Wanashika upinde na mkuki;Ni wakatili, hawana huruma;Sauti yao inanguruma kama bahari,Nao wamepanda farasi;Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani,Juu yako, Ee binti Babeli.

43. Mfalme wa Babeli amesikia habari zao,Na mikono yake imekuwa dhaifu;Dhiki imemshika, na maumivu,Kama ya mwanamke katika utungu wake.

Yer. 50