Yer. 46:2-12 Swahili Union Version (SUV)

2. Katika habari za Misri; habari za jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri, lililokuwa karibu na mto Frati katika Karkemishi, ambalo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, alilipiga katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda.

3. Tengenezeni kigao na ngao, mkakaribie ili kupigana.

4. Watandikeni farasi; pandeni, enyi mpandao farasi; simameni na chapeo zenu, isugueni mikuki; zivaeni dirii.

5. Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjika-vunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu ziko pande zote; asema BWANA.

6. Mtu mwepesi asikimbie, wala shujaa asiokoke; pande za kaskazini karibu na mto Frati wamejikwaa na kuanguka.

7. Nani huyu ajiinuaye kama mto Nile,Ambaye maji yake yanajirusha kama mito?

8. Misri anajiinua kama mto Nile,Na maji yake yanajirusha kama mito;Asema, Nitajiinua, nitaifunikiza nchi;Nitauharibu mji na hao wakaao ndani yake.

9. Haya! Pandeni, enyi farasi;Jihimizeni, enyi magari ya vita;Mashujaa nao na watoke njeKushi na Puti, watumiao ngao;Nao Waludi, washikao uta na kuupeta.

10. Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi,Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake;Nao upanga utakula na kushiba,Utakunywa damu yao hata kukinai;Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yakeKatika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.

11. Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.

12. Mataifa wamesikia habari za aibu yako, nayo dunia imejaa kilio chako; maana shujaa amejikwaa juu ya shujaa mwenzake, wameanguka wote wawili pamoja.

Yer. 46