Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi,Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake;Nao upanga utakula na kushiba,Utakunywa damu yao hata kukinai;Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yakeKatika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.