Yer. 43:8-13 Swahili Union Version (SUV)

8. Ndipo neno la BWANA likamjia Yeremia huko Tahpenesi, kusema,

9. Twaa mawe makubwa mikononi mwako, ukayafiche ndani ya chokaa ya kazi ya matofali, penye maingilio ya nyumba ya Farao huko Tahpanesi, machoni pa watu wa Yuda;

10. ukawaambie, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitatuma na kumtwaa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitaweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya niliyoyaficha; naye atatandaza hema yake ya fahari juu yake.

11. Naye atakuja, na kuipiga nchi ya Misri; watu walioandikiwa kufa watakufa, nao walioandikiwa kuwa mateka watakuwa mateka, nao walioandikiwa kupigwa kwa upanga watapigwa kwa upanga.

12. Nami nitawasha moto katika nyumba za miungu ya Misri, na kuziteketeza, na kuwachukua mateka; naye atajipamba kwa nchi ya Misri, kama vile mchungaji avaavyo nguo zake; naye atatoka huko na amani.

13. Naye atazivunja nguzo za Bethshemeshi, iliyoko huko katika nchi ya Misri, na nyumba za miungu ya Misri ataziteketeza.

Yer. 43