Yer. 29:17-22 Swahili Union Version (SUV)

17. BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitaleta juu yao upanga, na njaa, na tauni, nami nitawafanya kuwa kama tini mbovu, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana.

18. Nami nitawafuatia kwa upanga, na njaa, na tauni, nami nitawatoa watupwe huko na huko katika falme zote za dunia, wawe kitu cha kulaaniwa, na cha kushangaza, na cha kuzomewa, na cha kulaumiwa, katika mataifa yote nilikowafukuza.

19. Kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu, asema BWANA, ambayo naliwatuma watumishi wangu, hao manabii, nikiamka mapema, na kuwatuma; lakini hamkutaka kusikiliza, asema BWANA.

20. Basi, lisikieni neno la BWANA, ninyi nyote mliochukuliwa mateka, niliowapeleka toka Yerusalemu mpaka Babeli.

21. BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, katika habari za Ahabu, mwana wa Kolaya, na katika habari za Sedekia, mwana wa Maaseya, wawatabiriao ninyi maneno ya uongo kwa jina langu; Tazama, nitawatia katika mikono ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, naye atawaua mbele ya macho yenu.

22. Tena katika habari zao laana itatumiwa na wafungwa wote wa Yuda, walioko Babeli, kusema, BWANA akufanye uwe kama Sedekia, na kama Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwaoka motoni;

Yer. 29