13. Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.
14. Je! Israeli ni mtumwa? Je! Ni mzalia?mbona amekuwa mateka?
15. Wana-simba wamenguruma juu yake,wametoa sana sauti zao;Nao wameifanya nchi yake kuwa ukiwa;miji yake imeteketea, haina watu.
16. Tena wana wa Nofu na Tahpanesi wamevunja utosi wa kichwa chako.
17. Je! Hukujipatia mambo haya mwenyewe, kwa kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, alipokuongoza njiani?
18. Na sasa una nini utakayotenda katika njia iendayo Misri, kunywa maji ya Shihori? Au una nini utakayotenda katika njia iendayo Ashuru, kunywa maji ya ule Mto?
19. Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, BWANA wa majeshi.