16. Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa;Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote;Na Israeli ni kabila ya urithi wake;BWANA wa majeshi ndilo jina lake.
17. Haya! Kusanya bidhaa yako katika nchi, wewe ukaaye katika mazingiwa.
18. Maana BWANA asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu.
19. Ole wangu, kwa sababu ya jeraha yangu! Pigo langu laumia; lakini nalisema, Kweli, ni huzuni yangu mimi, nami sina budi kuivumilia.
20. Hema yangu umetekwa nyara, kamba zangu zote zimekatika; watoto wangu wameniacha na kwenda zao, pia hawako. Hapana mtu atakayenitandikia tena hema yangu, na kuyatundika mapazia yangu.
21. Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa BWANA; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika.