Wim. 5:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Naingia bustanini mwangu, umbu langu, bibi arusi,Nachuma manemane yangu na rihani,Nala sega la asali na asali yangu,Nanywa divai yangu na maziwa.Kaleni, rafiki zangu, kanyweni,Naam, nyweni sana, wapendwa wangu.

2. Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho,Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha!Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu,Hua wangu, mkamilifu wangu,Kwa maana kichwa changu kimelowa umande,Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.

3. Nimeivua kanzu yangu; niivaeje?Nimeitawadha miguu; niichafueje?

4. Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni,Na moyo wangu ukachomeka kwa ajili yake.

Wim. 5