Wim. 2:14-16 Swahili Union Version (SUV)

14. Hua wangu, mafichoni mwa jabali,Katika sitara za magenge,Nitazame uso wako, nisikie sauti yako,Maana sauti yako ni tamu na uso wako mzuri.

15. Tukamatie mbweha,Wale mbweha wadogo,Waiharibuo mizabibu,Maana mizabibu yetu yachanua.

16. Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake;Hulisha kundi lake penye nyinyoro.

Wim. 2