Wim. 1:7-16 Swahili Union Version (SUV)

7. Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu,Ni wapi utakapolisha kundi lako,Ni wapi utakapolilaza adhuhuri.Kwa nini niwe kama aliyefungiwa kidoto,Karibu na makundi ya wenzako?

8. Usipojua, wewe uliye mzuri katika wanawake,Shika njia uzifuate nyayo za kondoo,Na kuwalisha wana-mbuzi wakoKaribu na hema za wachungaji.

9. Mpenzi wangu, nimekulinganishaNa farasi katika magari ya Farao.

10. Mashavu yako ni mazuri kwa mashada,Shingo yako kwa mikufu ya vito.

11. Tutakufanyizia mashada ya dhahabu,Yenye vifungo vya fedha.

12. Muda mfalme alipoketi juu ya matakia,Nardo yangu ilitoa harufu yake.

13. Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemaneUkilazwa usiku maziwani mwangu.

14. Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina,Katika mizabibu huko Engedi.

15. Tazama, u mzuri, mpenzi wangu,U mzuri, macho yako ni kama ya hua.

16. Tazama, u mzuri, mpendwa wangu,Wapendeza, na kitanda chetu ni majani;

Wim. 1