1. Wimbo ulio bora, wa Sulemani.
2. Kubusu na anibusu kwa kinywa chake.Maana pambaja zako zapita divai;
3. Manukato yako yanukia vizuri;Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa;Kwa hiyo wanawali hukupenda.
4. Nivute nyuma yako, na tukimbie;Mfalme ameniingiza vyumbani mwake.Tutafurahi na kukushangilia;Tutazinena pambaja zako kuliko divai;Ndiyo, ina haki wakupende.
5. Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri,Enyi binti za Yerusalemu,Mfano wa hema za Kedari,Kama mapazia yake Sulemani.
6. Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi,Kwa sababu jua limeniunguza.Wana wa mamangu walinikasirikia,Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu;Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.