Ufu. 3:18-22 Swahili Union Version (SUV)

18. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19. Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20. Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21. Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Ufu. 3