1. Jinsi dhahabu ilivyoacha kung’aa,Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika!Mawe ya patakatifu yametupwaMwanzo wa kila njia.
2. Wana wa Sayuni wenye thamani,Walinganao na dhahabu safi,Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo,Kazi ya mikono ya mfinyanzi!
3. Hata mbwa-mwitu hutoa matiti,Huwanyonyesha watoto wao;Binti ya watu wangu amekuwa mkali,Mfano wa mbuni jangwani.
4. Ulimi wa mtoto anyonyayeWagandamana na kaakaa lake kwa kiu;Watoto wachanga waomba chakula,Wala hakuna hata mmoja awamegeaye.
5. Wale waliokula vitu vya anasaWameachwa peke yao njiani;Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekunduWakumbatia jaa.