12. Wao huwauliza mama zao,Zi wapi nafaka na divai?Hapo wazimiapo kama waliojeruhiwaKatika mitaa ya mji,Hapo walipomiminika nafsi zaoVifuani mwa mama zao.
13. Nikushuhudie nini? Nikufananishe na nini,Ee Binti Yerusalemu?Nikusawazishe na nini, nipate kukufariji,Ee bikira binti Sayuni?Kwa maana uvunjifu wako ni mkuu kama bahari,Ni nani awezaye kukuponya?
14. Manabii wako wameona maono kwa ajili yakoYa ubatili na upumbavuWala hawakufunua uovu wako,Wapate kurudisha kufungwa kwako;Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yakoNa sababu za kuhamishwa.
15. Hao watu wote wapitaoHukupigia makofi;Humzomea binti Yerusalemu,Na kutikisa vichwa vyao;Je! Mji huu ndio ulioitwa, Ukamilifu wa uzuri,Furaha ya dunia yote?