1. Jinsi Bwana alivyomfunika binti SayuniKwa wingu katika hasira yake!Ameutupa toka mbinguni hata nchiHuo uzuri wa Israeli;Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yakeKatika siku ya hasira yake.
2. Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo,Wala hakuona huruma;Ameziangusha ngome za binti YudaKatika ghadhabu yake;Amezibomoa hata nchiAmeunajisi ufalme na wakuu wake.