Omb. 1:9-11 Swahili Union Version (SUV)

9. Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake;Hakukumbuka mwisho wake;Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu;Yeye hana mtu wa kumfariji;Tazama, BWANA, teso langu;Maana huyo adui amejitukuza.

10. Huyo mtesi amenyosha mkono wakeJuu ya matamaniko yake yote;Maana ameona ya kuwa makafiri wameingiaNdani ya patakatifu pake;Ambao kwa habari zao wewe uliamuruWasiingie katika kusanyiko lako.

11. Watu wake wote hupiga kite,Wanatafuta chakula;Wameyatoa matamaniko yao wapate chakulaCha kuihuisha nafsi;Ee BWANA, tazama, uangalie;Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.

Omb. 1