1. Maono yake Obadia.Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu;Tumepata habari kwa BWANA,Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa,Akisema, Haya, inukeni ninyi;Na tuinuke tupigane naye.
2. Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa;Umedharauliwa sana.
3. Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,Wewe ukaaye katika pango za majabali,Mwenye makao yako juu sana;Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?
4. Ujapopanda juu kama tai,Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota,Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
5. Kama wevi wangekujilia, kama wanyang’anyi wangekujilia usiku, (jinsi ulivyokatiliwa mbali!) Je! Wasingeiba kiasi cha kuwatosha? Kama wachumao zabibu wangekujilia, je! Wasingeacha baadhi ya zabibu, ziokotwe?
6. Jinsi watu wa Esau wanavyotafutwa-tafutwa! Jinsi hazina zake zilizofichwa zinavyoulizwa-ulizwa!
7. Watu wote wa mapatano yakoWamekufukuza, hata mipakani;Wale waliofanya amani naweWamekudanganya, na kukushinda;Walao mkate wako wameweka mtego chini yako;Wala hana ufahamu wa hayo ndani yake.
8. Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika kilima cha Esau? Asema BWANA.
9. Na mashujaa wako, Ee Temani, watafadhaika, hata iwe kila mtu akatiliwe mbali kwa kuuawa katika kilima cha Esau.
10. Kwa sababu ya udhalimu aliotendwa ndugu yako Yakobo, aibu itakufunika, nawe utakatiliwa mbali hata milele.
11. Siku ile uliposimama upande, siku ile wageni walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kumpa kura juu ya Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao.