9. Tena Bakbukia na Uno, ndugu zao, kuwaelekea kwa zamu.
10. Naye Yoshua akamzaa Yoyakimu, Yoyakimu akamzaa Eliashibu, Eliashibu akamzaa Yoyada,
11. Yoyada akamzaa Yohana, Yohana akamzaa Yadua.
12. Na siku za Yoyakimu wakawako makuhani, wakuu wa mbari za mababa; wa Seraya, Meraya; wa Yeremia, Hanania;
13. wa Ezra, Meshulamu; wa Amaria, Yehohanani;
14. wa Maluki, Yonathani; wa Shekania, Yusufu;
15. wa Harimu, Adna; wa Meremothi, Helkai;
16. wa Ido, Zekaria; wa Ginethoni, Meshulamu;
17. wa Abia, Zikri; wa Miyamini; wa Maazia, Piltai;
18. wa Bilgai, Shamua; wa Shemaya, Yehonathani;
19. wa Yoyaribu, Matenai; wa Yedaya, Uzi;
20. wa Salu, Kalai; wa Amoki, Eberi;
21. wa Hilkia, Hashabia; wa Yedaya, Nethaneli.
22. Walawi siku za Eliashibu, na Yoyada, na Yohana, na Yadua, wameandikwa wakuu wa mbari za mababa; tena na makuhani; hata siku za kumiliki kwake Dario, Mwajemi.
23. Wana wa Lawi, wakuu wa mbari za mababa, wameandikwa katika kitabu cha tarehe, hata siku za Yohana mwana wa Eliashibu.
24. Nao wakuu wa Walawi; Hashabia, Sherebia, Yeshua, Binui, Kadmieli, na ndugu zao kuwaelekea, ili kusifu na kushukuru, kama amri ya Daudi, mtu wa Mungu, zamu kwa zamu.